WAZIRI GWAJIMA AIPONGEZA MCT KWA KUTUMIA MFUMO WA MONTESSORI KUFUNDISHA WATOTO

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akiwa na watoto wakizundua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) hafla iliyofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Montessori Community of Tanzania (MCT) , Martha Dello mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto uliofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akimsikiliza Mratibu Kanda ya Ziwa wa Montessori, Magdalena Telentine baada ya kutembelea banda hilo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto uliofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akionyeshwa mbinu mbalimbali zinazotumika kumfundishia mtoto na Mkurugenzi wa MCT, Sarah Kiteleja, baada ya kukagua banda hilo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto uliofanyika leo Desemba 13,2021 jijini Dodoma

Jamii imeshauriwa kutumia mfumo wa ufundishaji wa Montessori kwa kuwa unamsaidia mtoto kukua katika maisha na si kielimu peke yake.
Rai hiyo imetolewa leo Desemba 13,2021 na Mwenyekiti wa Montessori Community of Tanzania (MCT) , Martha Dello wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao la maonesho kwenye uzinduzi wa program jumuishi ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto uliofanyika jijini Dodoma.
Dello amesema mfumo huo una maeneo matano yanayosaidia kumkuza mtoto na kumuendeleza katika nyanja zote kwa vifaa na vitendo vya kawaida.
“Maria Montessori alisema ya kwamba hatuwezi kuwakinga watoto wetu na maisha, tunaweza kuwaandaa watoto wetu na maisha,kwenye darasa la Montessori tunatumia vifaa zaidi kama mnavyoona hapa, tuna maeneo matano yanayomkuza na kumuendeleza mtoto kuna vitendo vya kawaida.”
“Tunaposema vitendo vya kawaida ni vile vinavyofanyika kwenye maisha yetu ya kila siku kwa kufagia, kuosha vyombo vinamsaidia kujitegemea kuwajibika kwenye maisha yake…vitendo hivi baadaye vinamsaidia kwenye kuandika anakuza misuli yake, kuna vitendo vya milango ya fahamu,”amesema.
Amebainisha kuwa vitendo hivyo vya milango ya fahamu husaidia kubaini kama kuna mtoto ana tatizo na kupelekwa hospitali.
“Tunamfundisha mtoto lugha ni muhimu katika mawasiliano, mambo ni mengi katika Montessori kuna vyuo vinatoa mafunzo kwa mfumo huu, kuna madarasa ya awali yapo mikoa yote Tanzania yanafundisha kwa mfumo huu,”amesema.
Naye, Mkurugenzi wa MCT, Sarah Kiteleja, amesema mfumo huo unamsaidia mtoto kujitambua, kupata ujuzi na ujasiri wa kufanya vizuri kwenye maisha yake.
“Tunafanya kazi na jamii, tunahamasisha serikali iweze kuchukua mbinu hii ya ufundishaji ili kusaidia watoto wa kitanzania kuwa na weledi wa kufanya vizuri na kuwa na ubunifu,”amesema.
Alisema watoto wengi wa kitanzania wananyanyasika kutokana na malezi mabaya na kwamba mfumo huo unamponya na kuwa na utu.
Kwa upande wake, Mratibu Kanda ya Ziwa wa Montessori, Magdalena Telentine, amesema mfumo huo unampa mtoto mwenye umri wa miaka sita kujifunza vitu vingi kwa wakati mmoja kutokana na kuzaliwa na akili sharabifu(akili yenye uwezo wa kubeba kila kitu kilichopo kwenye mazingira yake).
Amesema ujifunzaji wa mtoto mdogo ni tofauti na mkubwa na kwamba kwa umri huo mtoto anapaswa kupewa kila kitu kilichopo kwenye mazingira yake.
“Katika kuwalea watoto tujitahidi kuwaweka mbali na vitu vibaya kwa kuwa umri huo mtoto hana uwezo wa kuchanganua hili jema au baya, huu mfumo unamsaidia kumjenga mtoto kiroho, kimwili, kiakili na kiutamaduni, na mbinu hii haiishii kwa umri huo bali inaenda hadi elimu ya msingi,”amesema.

138 Comments

  1. Разрешение на строительство — это административный акт, выдаваемый авторизованными ведомствами государственной власти или местного руководства, который дает возможность начать строительство или исполнение строительных работ.
    Разрешение на строительство на строящийся объект устанавливает законодательные положения и требования к строительным работам, включая узаконенные разновидности работ, приемлемые материалы и способы, а также включает строительные стандарты и пакеты защиты. Получение разрешения на строительные операции является обязательным документов для строительной сферы.

  2. Быстровозводимые здания – это современные здания, которые отличаются большой скоростью строительства и мобильностью. Они представляют собой постройки, состоящие из заранее произведенных составляющих или узлов, которые могут быть скоро установлены на участке стройки.
    Быстровозводимые здания из сэндвич панелей проекты стоимость отличаются податливостью и адаптируемостью, что разрешает легко менять и модифицировать их в соответствии с потребностями клиента. Это экономически эффективное и экологически стойкое решение, которое в крайние лета получило обширное распространение.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *